Serikali ya Libya inayotambulika kimataifa imesema inapanga kufungua katika taifa la kigeni akaunti ya benki kwa ajili ya kuhifadhi mapato ya mafuta. Hatua hiyo inalenga kuzuwiya mapato ya sekta hiyo yasingie kwenye mikono ya serikali pinzani ya nchi hiyo yenye makao yake mjini Tripoli. Mapato ya mafuta yasiyosafishwa ndiyo chanzo cha vita vya kuwania udhibiti wa taifa hilo la Afrika Kaskazini mwanachama wa nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi - OPEC, ambavyo vinazihusisha kambi mbili hasimu na vikosi vya wapiganaji vinavyowaunga mkongo vimekuwa vikipambana kwa miaka minne baada ya kuanguka kwa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi. Serikali ya Waziri Mkuu Abdullah al- Thinni ambayo ina makao yake mashariki mwa Libya, imetoa maelezo ya mfumo mpya wa malipo ya sekta ya mafuta, lakini wachambuzi wanasema huenda ikashindwa kuwashawishi wafanyabiashara wa kimataifa kuwa inaweza kudai umiliki wa halali wa mafuta yasiyosafishwa ya Libya. Thinni ameliamuru Shirika la Kitaifa la Mafuta la serikali yake kufungua akaunti tofauti katika Umoja wa Falme za Kiarabu sambamba na Shirika la Mafuta la Taifa (NOC) ambalo limekataa kujihusisha katika mzozo baina ya serikali hizo mbili hasimu.
5 Aprili 2015 - 20:54
Msimbo wa Habari: 681463
Serikali ya Libya inayotambulika kimataifa imesema inapanga kufungua katika taifa la kigeni akaunti ya benki kwa ajili ya kuhifadhi mapato ya mafuta.